• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa warefusha muda wa kupeleka misaada nchini Syria kwa mwaka mmoja

    (GMT+08:00) 2016-12-22 09:28:56

    Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio la kurefusha muda wa kupeleka misaada kwa kuvuka mipaka nchini Syria kwa mwaka mmoja hadi mwezi Januari mwaka 2018.

    Nchi 15 wajumbe wa Baraza la Usalama zimeonesha kukasirishwa na hali isiyokubalika ya kuongezeka kwa vurugu na kuwaua kwa watu zaidi ya laki 2.5 kwenye mgogoro nchini Syria. Hivyo baraza hilo limeitaka serikali ya Syria iitikie maombi yote ya Umoja wa Mataifa na washirika wake kwa ajili ya kufikisha misaada kwa wenye mahitaji nchini humo.

    Baraza la usalama pia limeamua kutuma waangalizi wa Umoja wa mataifa kusimamia mchakato wa kuondoka kwa maelfu ya watu waliokwamba mjini Allepo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako