• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kibarua cha Alan Pardew chaota mbawa Crystal Palace

    (GMT+08:00) 2016-12-23 08:54:11

    Klabu ya Crystal Palace imemfuta kazi mkufunzi wake Alan Pardew wakati ambapo klabu hiyo iko katika nafasi ya 17 katika ligi ya Uingereza.

    Pardew aliteuliwa na kupewa mkataba wa miaka mitatu na nusu uliotiwa sahihi mnamo mwezi Januari 2015, lakini meneja huyo mwenye umri wa miaka 55 amefukuzwa kazi baada ya kushinda mechi moja pekee kati ya 11. Palace imejipatia pointi 26 katika mechi 36 ilizocheza 2016 na ina pointi moja tu juu ya timu zilizo katika hatari ya kushushwa daraja.

    Aliyekuwa kocha wa Uingereza Sam Allardyce anapigiwa upatu kuchukua wadhfa huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako