• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Usalama kuimarishwa katika sherehe za krismasi Kenya

    (GMT+08:00) 2016-12-23 09:42:08

    Wizara ya usalama wa kitaifa nchini Kenya imewakikishia wakenya wote usalama wa kutosha na hali ya utulivu na amani wakati wa sherehe za krismasi zitakazofanyika tarehe 25 Mwezi huu.

    Kamati za usalama zimeundwa katika kaunti zote nchini Kenya ili kupiga doria za kuimarisha usalama pamoja na kukabiliana na uhalifu wa aina yoyote.

    Mgeni njoo mwenyeji apone,ni wakati mwengine wa msimu wa krismasi ,waumini wa dini ya kikristo kote duniani wanajitayarisha kuandaa sherehe za kukata na shoka mwaka huu.

    Serikali ya Kenya imeanza doria ya mapema kuhakikisha wakenya wote watakuwa na amani na utulivu kwa kubuni vikosi vitakavolinda usalama .

    Mratibu mkuu wa idara ya usalama katika kaunti ya Mombasa Nelson Marwa amesema msimu huu wametumia mbinu mpya za kuhakikisha wahalifu hawapati nafasi ya kuvuruga usalama.

    "Tunatarajia wageni wengi kutoka nchi za nje na hapa nchini kufika Mombasa kwa krismasi,tumeweka mikakati kabambe ya kiusalama"

    Kamishena wa kaunti ya Mombasa Evans Achoki nae ameshinikiza kwamba kikosi maalum kitakachovalia sare za kawaida kama raia kitatawanyika katika sehemu zote za utalii ikiwemo fuo za bahari.

    "Tunajua kuhusu vijana wanaojaribu kuleta hali za taharuki wakati huu wa sherehe lakini ole wako ukipatikana na hatia,hatutaki visa vovote vya uhalifu wala ugaidi"

    Tana River,Lamu,Malindi,Diani na Kwale ni baadhi ya maeneo yatakokuwa na ulinzi mkali kutokana na visa vya mashambulizi ya ugaidi vilivowahi kutokea huko nyuma.

    Jeshi la ulinzi la KDF litaendelea na oparesheni ya kulinda sehemu za mipaka ya Kenya na Somalia wakati wote wa sherehe hizi.

    Huku idadi kubwa ya wakenya ikiendelea na pilka pilka za kusafiri kuelekea mashambani,halmashauri ya kitaifa ya usimamizi wa barabara nchini imetoa onyo kali kwa madereva wa magari ya umma nay a kibinafsi dhidi ya kuvunja sheria za barabarani.

    Halmashauri hiyo imetangaza kuchukua hatua kali za kisheria kwa watumizi wa barabani watakokiuka kanuni pamoja na kutoa thadhari kwa madereva walevi kufunguliwa mashtaka.

    Mwezi huu wa Disemba visa vya ongezeko la ajli vimeongezeka maradufu na kusababisha vifo vya idadi kubwa ya watu kimoja cha hivi karibuni ikiwa ni ajali ya eneo la Naivasha ambapo watu zaidi ya 40 walipoteza maisha.

    Kama kawaida sekta ya uchukuzi wa umma imepandisha nauli ya usafiri kwa viwango vikubwa kutokana na mafuriko ya watu kwenye vituo vya kuabiri magari ya mashinani.

    "nauli iko juu sana,Ningeomba upande wa serikali kudhibiti jambo hili"

    Wafanyibiashara wa bidhaa kama chakula na zawadi wana furaha kupita maelezo kwani mauzo yamepanda sihaba

    "Nimekuja kununua mapema vitabu kwa sababu januari kutakuwa na watu wengi bei itapanda"

    Watalii waliowasili nchini kwa sherehe hizi wanatarajia kujivinjari ipasavyo na kula kuku kwa mrija ufuoni.

    Wakenya hawakuachwa nyuma nao kwani kama wanavosema wamejiandaa kujienjoy vilivyo haswa baada ya mwaka mzima wa kazi ngumu na majukumu

    "Tunaelekea wakati wa krismasi tuko hapa sokoni tunatafuta vitu ni wakati wa kwenda nyumbani na tunanunua zawadi

    "Krsimasi ni wakati wa kukutana pamoja na jamii zao ,na pia tunasherekea pamoja kwa chakula"

    Radio China inawakatia wote krismasi njema na kufana na kufaana.

     

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako