• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ndege ya jeshi la Russia yaanguka kwenye bahari nyeusi na kuua abiria wote

    (GMT+08:00) 2016-12-26 09:08:08

    Ndege ya jeshi la Russia aina ya Tu-154 imeanguka kwenye bahari nyeusi na kusababisha vifo vya watu 92.

    Ndege hiyo iliyokuwa inaenda kwenye kambi ya jeshi la anga ya Hmeimim katika mji wa Latakia nchini Syria, ilipotea kwenye rada muda mfupi baada ya kuruka kutoka mji wa Sochi. Baadhi ya miili ya wahanga imepatikana kwenye eneo la ajali, na mabaki ya ndege yamepatikana kwenye eneo lenye kipenyo cha kilometa 1.5 na kina cha hadi mita sabini baharini.

    Watu zaidi ya elfu 3,000 wakiongozwa na waziri wa Ulinzi wa Russia Bw Sergei Shoigu wamepelekwa kwenye eneo la tukio kwa ajili ya usakaji na uokoaji.

    Habari zinasema chanzo cha ajali ya ndege hiyo iliyotengenezwa mwaka 1983 na kufanyiwa marekebisho ya kiufundi mwezi Septemba, inawezekana kuwa ni hitilafu za kiufundi au makosa ya rubani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako