• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Msako wa NTSA msimu huu wa sherehe

    (GMT+08:00) 2016-12-26 09:45:45

    Mamlaka ya Kitaifa ya Usalama na Usafiri ( NTSA) imeanza msako mkali kwa magari ya kibinafsi yaliogezwa na kuwa ya abiria wakati huu wa msimu wa sherehe.

    NTSA imesema hatua hii ni ya kupunguza ajali zinazohusika na magari ya kibinafsi barabarani, hasa wakati huu.

    Watu wakiwa katika pilikapilika za kuvuka mwaka mpya, mambo mengi yafanyika katika sekta usafiri.

    Mamlaka ya usalama na usafiri imechukua jukumu la kulinda wananchi katika barabara, ikishuhudiwa miaka ya nyuma watu wengi walipoteza maisha na wengi kujeruhiwa vibaya kutokana na kutokuwa makini barabarani.

    Msimu huu watu wengi usafiri kujumuika na familia zao maeneo mbali mbali, na wakati mwengi magari ukosekana hivyo vutia magari ya kibinafsi.

    "Wajuawa kuto kuelewa alafu vile sahi ni hii msimu magari iko kidogo sana, hivyo inabidii tupande magari binafsi"

    Mwishoni mwa wiki iliyopita NTSA ilishika magari kumi ya kibinafsi yalikuwa yakiopareti kama magari ya abiri.

    NTSA imeahidi kuendelea na msako wa magari hata baada ya msimu huu wa krismasi na mwaka mpya.

    "Hazijafikia viwango vinavyoitajika kuweza kuhudumu kama gari za abiri na ndio maana NTSA inachukua hii nafasi kuhakikisha magari kama haya haziko kwa barabara"

    Kulingana NTSA magari ya kibinafsi yanayofanya kazi kinyume cha sheria yamechangia ongezeko la aslimia 34 ya ajali mbaya barabarani mwaka huu, ikilinganishwa na asilimia 21 ya gari za abiri.

    "Gari za kibinafsi ndizo zinazoongoza vifo katika barabara zetu kwa asilimia 34 zikifutwa na magari ya biashara ambayo karibu asilimia 24 kisha magari ya utumishi wa umma 21."

    Hapo nyuma magari ya abiri ndiyo yalikuwa yanaongoza katika ajali barabarani, lakini tangu kuanzishwa kwa vithibi mwendo ajali zimepungua.

    Inspeta generali Joseph boinnet anasema msako huu utaendelea hasa kwa magari, kama Noah, probox na toyota wish ambazo zinatumika kama gari za abiri kubeba watu.

    Hii imetokana na malalamishi kutoka kwa madereva wa gari za abiri, wakisema biashara ya magari binafsi kusafirisha abiri inasababisha ushindani usio wa haki.

    Msako wa magari ya kibinafsi yanayosafirisha watu utaendelea katika barabara zote kuu katika msimu huu wa sherehe.

    Polisi wameshirikiana na mamlaka ya usalama na usafiri (NTSA) kumkamata mtu yeyote atakevuja sheria za barabarani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako