• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu tisa wafariki dunia kwenye ajali ya boti ziwa Albert magharibi mwa Uganda

    (GMT+08:00) 2016-12-27 08:35:14

    Watu tisa wamefariki dunia na wengine 36 wamenusurika kwenye ajali ya boti iliyotokea jumapili kwenye ziwa Albert katika wilaya ya Buliisa magharibi mwa Uganda.

    Kamanda wa polisi wa Wilaya Buliisa Bw John Rutaagira amesema ajali hiyo ilitokea mita 100 baada ya boti hiyo kuondoka bandarini, ambapo upepo mkali uliikumba boti hiyo iliyokuwa na abiria 45, ambao ni wengi kuliko uwezo wake.

    Kamanda huyo pia amesema abiria wa boti hiyo walikuwa wanasafiri kwenda kwenye mechi ya soka kwenye wilaya ya Hoima, wote walikuwa ni wanaume waliokuwa wamelewa, na hakuna hata mmoja aliyekuwa na boya la kuwasaidia kuelea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako