• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kifaa cha kurekodi safari ya ndege ya Russia iliyoanguka chapatikana

    (GMT+08:00) 2016-12-27 19:04:55

    Wizara ya ulinzi ya Russia imesema, kifaa cha kurekodia safari ya ndege ya kijeshi ya Russia iliyoanguka kwenye Bahari Nyeusi kimepatikana katika mabaki ya ndege hiyo.

    Kifaa hicho ambacho pia kinajulikana kama kisanduku cheusi, kitapelekwa kwenye idara ya uchunguzi ya Jeshi la Anga la Russia ili wataalam waweze kuchukua taarifa zilizorekodiwa.

    Wizara hiyo imesema, operesheni ya uokoaji katika eneo ilipotokea ajali hiyo imeendelea, na mpaka sasa, jumla ya miili 12 imepatikana na sehemu mbalimbali za viungo pia zimepatikana na kupelekwa mjini Moscow kwa ajili ya utambuzi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako