• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wilfred Ndindi aripotiwa kukaribia kujiunga na Leicester City

    (GMT+08:00) 2016-12-28 08:35:17

    Kiungo wa kimataifa wa Nigeria anayeichezea KRC Genk ya Ubelgiji Wilfred Ndindi ameripotiwa kukaribia kujiunga na Leicester City January 1 2017. Habari kutoka express.co.uk zinasema Ndindi tayari amekamilisha uhamisho wake wa kujiunga na Leicester City na kinachosubiriwa ni kutangazwa rasmi January 1 2017. Mchezaji huyo anajiunga na Leicester City kwa dau la pound milioni 15. Ndindi amecheza jumla ya mechi 33 akiwa na Genk na kufunga magoli matatu. Mnigeria huyu anakwenda kuziba pengo la Ng'olo Kante aliyejiunga na Chelsea. Mtu wa karibu na Ndindi amenukuliwa na express.co.uk kuwa Ndindi kacheza mchezo wa mwisho akiwa na Genk dhidi ya KAA Gent na atasafiri January 1 kwenda kufanya vipimo, habari ambazo zinapata uzito kutokana na baadhi ya mashabiki wa Genk wa instagram kuanza kumuaga. Ndindi pia alikuwa anawaniwa na Man United.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako