• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wizi wa mifugo Kenya wakithiri wakati huu wa msimu wa sherehe

    (GMT+08:00) 2016-12-28 09:01:46

    Wizi wa mifugo nchini Kenya umekithiri hasa wakati huu wa msimu wa sherehe huku polisi wakiongeza doria kwenye maeneo yalioathrika.

    Polisi wamefanikiwa kupata zaidi ya mifugo 140 waliokuwa wameibiwa kutoka eneo la Gilgil na ambao walikuwa wanapelekwa kuchinjwa katika eneo la Dagoreti mjini Nairobi.

    Ronald Mutie anaripoti.

    Zaidi ya watu 6000 wametoroka maeneo ya Kiserian kaunti ya Baringo nchini Kenya wakihofia maisha yao kufuatia mashambulizi ya wezi wa mifugo.

    Sasa wamepiga kambi mbali na kwao wasirudi tena nyumbani.

    "Kuna vijana wamekuja kwa wingi, wanatembea huku na kila mtu ako na silaha yake na hatuwezi tukajua ni nini itafanyika." Anasema mmoja wa wakaazi.

    Wengi wa wale waliokimbia wamepiga kambi nje ya vituo vya polisi lakini pia washukiwa wameweka vizuizi barabarani ili kuzuia maafisa wa polisi kuwafikia waathiriwa.

    Sasa wanamtaka mkuu wa Polisi kuzuru eneo lao ili kusaidia kutuliza hali na kurejesha amani.

    Ndani ya mwezi huu wa Desemba kumekuwa na zaidi ya matukio 5 makubwa ya wizi wa mifugo katika maeneo mbali mbali hasa kaunti za Baringo, Nakuru na Transmara.

    Siku ya mkesha wa Krismasi zaidi ya mifuo 140 waliibiwa katika eneo la Gilgil kaunti ya Nakuru lakini kufuatia msako wa polisi wakapatikana katika eneo la Kamangu kaunti ya Kiambu waKIpelekwa kuchinjwa katika eneo la Dagoreti mjini Nairobi.

    Wakulima waliokuwa wamepoteza mifugo hao sasa wanalalamika kwa polisi waliokuwa wanashidka doria barabarani wakati wifugo waliposafirishwa usiku.

    Huyu hapa ni mmpja wa wale waliokuwa wamepoteza mifugo wao.

    "Ng'ombe wametoka Nakuru wamesafirishwa na kupitia kwa vizuizi vya barabarani katibu saba, na askari wako na hawawezi kuchunguza hao ng'ombe wanaenda wapi usiku. Sheria inasema ikifika saa kumi na mbili hakuna ruhusa ya kusafirisha ng'ombe."

    Polisi pia wamekuwa na kazi ngumu kuwakabili wezi hao.

    Wiki iliopita katika eneo la Tiaty kaunti ya Baringo wezi walichoma moto lori moja la polisi baada ya polisi hao kushindwa nguvu anasema mkuu wa polisi kwenye eneo hilo.

    Lakini hata hivyo serikali imepiga hatua za kukabili tatizo hili kwa kuwashirikisha wananchi wa pande zote zinazoibiana mifugo.

    Inspekta wa Polisi Jenerali Joseph Boinet anasema kwa sababu kila upande una malamiko yao, kwanza wanafaa kukomesha wizi, uharibifu wa mali na mauaji ili kuanza mazungumzo ya amani ya kudumu.

    "Ule mfano mwema ambao wananchi wa eneo hili wamefanya kurudisha amani, iingwe na wananchi wa Tiaty na Marakwet kwa sababu sisi zote tunataka amani"

    Boinet alisema serikali itazawadia kamati za amani ambazo zitachangia kurejea kwa amani ya kudumu kwenye maeneo yalioathirika.

    Anasema, "Kazi ya kuchukua makurutu wa polisi ilikuwa imeanza, lakini nimeamuru kamanda wa eneo hili asubiri kidogo ili tuhakikishe kwamba wale vijana ambao wamekuwa wakipigania amani wanakuwa ndani"

    Viongozi wa kisiasa pia wameahidi kushirikiana ili kukomesha wizi wa mifugo kwenye maeneo yao.

    Wizi wa mifugo huchangiwa na kugombania malisho, biashara haramu ya mifugo, kulipisa kisasi na utamaduni wa tangu jadi wa jamii husika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako