• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uturuki na Russia zafikia makubaliano kuhusu usimamishwaji vita nchini Syria

    (GMT+08:00) 2016-12-29 10:09:29

    Vyombo vya habari vya Uturuki vimetangaza kuwa Uturuki imefikia makubaliano na Russia kuhusu mpango wa kusimamisha vita kote nchini Syria leo usiku wa manane.

    Shirika la habari la Uturuki Anadolu limesema kuna mpango huo wa kusimamisha vita utatekelezwa kwa hatua mbili, ya kwanza ni kujitahidi kutimiza usimamishwaji vita kote nchini Syria, ya pili ni kuhimiza mazungumzo kati ya serikali ya Syria na makundi ya upinzani chini ya usuluhishi wa Ututuki na Russia.

    Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Bw Mevlut Cavusoglu amesema Uturuki na Russia zimeandaa makubaliano mawili kuhusu usimamishwaji vita nchini Syria na utatuzi wa kisiasa wa suala la nchi hiyo. Ameongeza kuwa Syria inatarajiwa kusitisha vita kwa muda mrefu na hatimaye kufikia utatuzi wa kisiasa wa suala lake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako