• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Zambia kununua meli za mizigo kwa ajili ya bandari ya Mpulungu

    (GMT+08:00) 2016-12-30 08:59:05

    Serikali ya Zambia inapanga kununua meli za mizigo kwa ajili ya bandari ya Mpulungu iliyoko kaskazini mwa nchi hiyo, ili kurahisisha usafirishaji wa watu na mizigo.

    Waziri wa mawasiliano na uchukuzi wa Zambia Bw. Brian Mushimba amesema, ununuzi wa meli za abiria na mizigo utasaidia kuhimiza uuzaji wa bidhaa za nchi hiyo kwenye kanda ya Maziwa makuu.

    Amesema hivi sasa meli zote zinazotumiwa kusafirisha mizigo kwenye kanda ya maziwa makuu zinamilikiwa na wawekezaji wa nje. Ameongeza kuwa, ununuzi huo unatarajiwa kufanyika mwakani baada ya kukarabatiwa upya kwa bandari hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako