• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la Iraq lawaua wapiganaji 200 wa kundi la IS kwenye operesheni mpya ya kuukomboa Mosul

    (GMT+08:00) 2016-12-30 11:14:10

    Jeshi la usalama la Iraq jana limetwaa tena mtaa mmoja na vijiji viwili, na kuwaua wapiganaji 200 wa kundi la Islamic State baada ya askari wa jeshi hilo kuanza operesheni ya pili kuwaondoa wapiganaji wa kundi hilo kutoka Mosul.

    Askari wa kupambana na ugaidi wamewashambulia wapiganaji walioko mstari wa mbele wa kundi la Islamic State kwenye mitaa kadhaa mashariki mwa Mosul, na kuamua kuudhibiti mtaa wa al-Quds wakati mapambano makali yanaendelea kwenye mtaa wa jirani.

    Kwenye upande wa kaskazini, askari wa jeshi la Iraq walikomboa kijiji cha al-Sada na kijiji cha Tawiyla na kupandisha bendera ya Iraq kwenye jengo kuu baada ya kupambana vikali na wapiganaji wa kundi la Islamic State.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako