• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Russia yalaani uamuzi wa vikwazo wa Marekani

    (GMT+08:00) 2016-12-30 18:32:38

    Katibu wa idara ya mawasiliano ya ikulu ya Russia Dmitri Peskov jana huko Moscow amesema, nchi hiyo inailaani Marekani kwa kuweka vikwazo zaidi dhidi ya Russia.

    Bw. Peskov amesema, hii inaonesha kuwa sera ya kidiplomasia ya Marekani ni ya kushambulia, na kwamba hatua hiyo ya Marekani itaharibu uhusiano kati yake na Russia, pia italeta athari kubwa kwa sera ya kidiplomasia ya rais mteule wa Marekani Donalad Trump.

    Bw. Peskov amesema, Russia pia itachukua hatua ya kufanana na Marekani. Vilevile amesema Marekani hivi sasa iko kipindi cha mpito wa madaraka, hivyo Russia inazitaka nchi hizo mbili ziweze kuchukua hatua za pamoja ili kuufanya uhusiano kati ya nchi hizo mbili uwe kawaida.

    Waziri wa mambo ya nje wa Russia ametoa pendekezo kwa rais Putin kuhusu kuwafukuza wanadiplomasia 35 wa Marekani nchini Russia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako