• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Russia kutowafukuza wanadiplomasia wa Marekani nchini Russia

    (GMT+08:00) 2016-12-31 17:15:52

    Russia imesema haitawafukuza wanadiplomasia wa Marekani nchini humo, baada ya Marekani kuwafukuza wanadiplomasia 35 wa Russia nchini mwake.

    Rais Putin amesema, wanadiplomasia wa Marekani nchini Russia watasherehekea sikukuu ya mwaka mpya pamoja na familia yao nyumbani. Pia amewaalika watoto wa wanadiplomasia hao kwenda ikulu ya Russia kusherehekea sikukuu kwa pamoja, vilevile amewatakia rais Barack Obama na rais mteule Donald Trump sikukuu njema.

    Amesema, kitendo hicho cha rais Obama ni cha kichochezi na kimekwenda kinyume na maslahi ya watu wa nchi hizo mbili na kuweza kuharibu uhusiano kati yao. Russia na Marekani zinawajibika majukumu ya kuhakikisha usalama wa dunia, lakini, kitendo hicho cha Marekani kimevunja mfumo mzima wa uhusiano wa kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako