• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China atoa salamu za pongezi za mwaka mpya wa 2017

    (GMT+08:00) 2016-12-31 19:23:59


    Wakati mwaka mpya unapowadia, kupitia Radio China Kimataifa CRI, Radio ya serikali kuu ya China CNR, Televisheni ya taifa ya China CCTV na kupita tovuti mbalimbali Rais Xi Jinping wa China anatoa salamu za heri ya mwaka mpya wa 2017. Ifuatayo ni hotuba nzima ya salamu za mwaka mpya za Rais Xi.

    Ndugu,Marafiki, Mabibi na Mabwana:

    Mwaka 2016 utapita, na kengele ya mwaka mpya inakaribia kugonga. Wakati tunapoaga mwaka 2016 na kuukaribisha mwaka mpya 2017, ningependa kutoa salamu za heri ya mwaka mpya kwa wananchi wa makabila yote, ndugu wa mikoa ya utawala maalumu ya Hong Kong na Macao, ndugu wa Taiwan na wachina wanaoishi katika nchi mbalimbali, pamoja na watu wa nchi na sehemu mbalimbali duniani.

    Kwa wananchi wa China, mwaka 2016 si mwaka wa kawaida ambao hatuwezi kuusahau, ambapo "Mpango wa 13 wa maendeleo ya miaka mitano" ulianza kutekelezwa, na kupata mafanikio. Tulifuata kwa vitendo wazo jipya kuhusu kazi za kujiendeleza, kuharakisha mchakato wa kufanikisha ujenzi wa jamii yenye maisha bora kwa pande zote, na kuhimiza ongezeko la ukuaji wa uchumi wa China liendelee kuwa mbele duniani. Tulijitahidi kuendeleza zaidi mageuzi kwa pande zote, na kupiga hatua kubwa katika kuufanyia mageuzi muundo wa utoaji bidhaa na huduma, mageuzi kwenye sekta ya ulinzi wa taifa na jeshi yamepata maendeleo makubwa, na mageuzi kwenye sekta nyingine za msingi yameamuliwa kimsingi. Tumesukuma mbele utawala wa nchi kwa mujibu wa sheria, kuimarisha mageuzi kwenye mfumo wa sheria, kuhimiza kwa nguvu utendaji haki kwenye mambo ya sheria na mahakama, na kulinda usawa na haki kwenye jamii. Tumejitahidi kusimamia Chama kwa nidhamu kali kwa pande zote, kuendelea kupambana kithabiti na ufisadi, kuendelea kusafisha mazingira ya kisiasa, na mienendo ya Chama, siasa na jamii imendelea kuboreshwa.

    Mwaka 2016, darubini kubwa zaidi inayojulikana kama "Macho ya Anga ya China" ilianza kufanya kazi, satellite ya utafiti ya "Wukong" ilizunguka kwenye mzunguko wake katika anga ya juu kwa mwaka mmoja, satellite ya kwanza duniani ya Quantum ya "Mozi" iliingia kwenye anga ya juu, chombo cha Shenzhou 11 na maabara ya anga ya juu ya Tiangong 2 vilisafiri kwenye anga ya juu, wanamichezo wa China walipata mafanikio kwenye mashindano ya Olimpiki, na timu ya mpira wa wavu ya wanawake ya China ilipata medali ya dhahabu kwa mara nyingine kwenye michezo ya Olimpiki baada ya miaka 12. Na vilevile, kutokana na mageuzi, tumerahisisha utaratibu wa kuwapatia wanavijiji wanaoishi mijini huduma kama wakazi wa mijini, mazingira ya shule kwenye sehemu nyingi maskini yameboreshwa, raia wanaweza kuomba vitambulisho vya ukazi kwenye sehemu wanazoishi, watu wasio na vitambulisho vya ukazi wa muda mrefu wameweza kuandikishwa na kupata vitambulisho, watu wengi wamepata madaktari wa nyumbani, na kila mto utakuwa na msimamizi wake... hayo yote yanaturidhisha.

    Mwaka 2016, katika kando ya ziwa Xizi, tulifanya mkutano wa 11 wa viongozi wa nchi za kundi la G20, ambapo mbali na busara na mipango ya China, pia tulionesha sura nzuri ya China kwa dunia. Ujenzi wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja" ulihimizwa kwa kasi, na Benki ya Uwekezaji wa Miundombinu ya Asia AIIB imeanza rasmi kufanya shughuli zake. Tumeshikilia kujiendeleza kwa amani, kulinda kithabiti mamlaka na ukamilifu wa ardhi pamoja na maslahi yetu baharini, na kwamba wananchi wa China hawakubali kitendo chochote chenye nia mbaya katika masuala hayo.

    Katika mwaka huu, maafa ya kimaumbile na matukio ya kiusalama vilitokea katika sehemu mbalimbali, na kusababisha hasara kubwa kwa maisha na mali za watu pamoja na shughuli za uzalishaji, tumehuzunika na kusikitika sana. Askari kadhaa wa kikosi cha kulinda amani cha China walijitolea mhanga kwa ajili ya amani ya dunia, tunawakumbuka na tutawahudumia vizuri jamaa zao.

    Mwaka 2016, tuliadhimisha kwa shangwe miaka 95 ya kuanzishwa kwa Chama cha Kikomunisti cha China, kuadhimisha miaka 80 ya ushindi wa Safari Ndefu ya Jeshi Jekundu la China, na tunapaswa kuwakumbuka kwa moyo wazee waliotoa michango yao kwa wananchi na taifa la China, kutosahau sababu ya kuanza safari yetu na kuendelea kusonga mbele.

    Ndegu zangu, Marafiki, Mabibi na Mabwana!

    "Mwaka unaopita na mwaka unaokuja vinapokezana, maendeleo yanapatikana siku hadi siku". Katika mwaka 2017 unaokuja, Chama cha Kikomunisti cha China kitafanya mkutano wake mkuu wa 19 wa wajumbe wote, ambapo tutafanya juhudi zetu kubwa zaidi kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa jamii yenye maisha bora kwa pande zote, kuimarisha mageuzi kwa pande zote, kutawala nchi kwa mujibu wa sheria, na kusimamia Chama kwa pande zote na kwa nidhamu kali. Matunda hayapatikani bila jasho, ni kwa kufanya juhudi tu ndipo tutakapoweza kutimiza matumaini yetu.

    Mtu yeyote hapaswi kuachwa katika mchakato wa kujenga jamii yenye maisha bora. Katika mwaka 2016 unaopita, watu maskini milioni 10 zaidi walifanikiwa kuondokana na umaskini, natoa shukrani zangu kwa wenzetu walio mstari wa mbele katika vita dhidi ya umaskini, wametoa jasho jingi. Wakati mwaka mpya unapowadia, nawakumbuka zaidi watu wenye shida, nataka kujua wanakula nini, wanaishi vipi, na kama wanaweza kusherehekea vizuri mwaka mpya na sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China au la. Pia najua baadhi ya wenzetu bado wana shida katika kutafuta nafasi za ajira, elimu ya watoto, huduma za matibabu na nyumba, na ni wajibu usiokwepeka kwa Chama na serikali kutatua matatizo hayo. Chama na jamii yetu zinapaswa kuendelea kuwajali na kuwasaidia watu maskini na wale wenye matatizo, ili kuwawezesha raia wengi zaidi wanufaike na matunda ya maendeleo ya mageuzi na kufanya maisha ya wananchi yawe mazuri zaidi.

    "Ushindi utapatikana kama viongozi na raia wakishirikiana" Iwapo sisi watu bilioni 1.3 tunashikamana, kama Chama chetu kitakuwa pamoja na wananchi daima, na wote tunafanya juhudi kwa bidii, hakika tutaweza kufanikisha safari yetu ndefu.

    Ndugu zangu, Marafiki, Mabibi na Mabwana!

    Wachina siku zote wanaona "dunia ni kama familia". Wananchi wa China sio tu wanataka kujipatia maendeleo yao wenyewe, bali pia wanatarajia watu wa nchi nyingine waishi maisha mazuri. Hivi sasa, vita dhidi ya umaskini bado inasumbua baadhi ya nchi na sehemu, maradhi na maafa pia vinawakabili watu wengi. Natarajia kwa moyo wa dhati kuwa jumuiya ya kimataifa itashirikiana na kufuata wazo la jumuiya ya binadamu kujitahidi kujipatia maendeleo kwa pamoja, na kujenga dunia yetu kuwa ya amani na ustawi zaidi.

    Tuwe na imani na matarajio zaidi na kukaribisha kwa pamoja kengele ya mwaka mpya.

    Asanteni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako