• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hotuba ya Mkuu wa Radio China Kimataifa kwa ajili ya Sikukuu ya Mwaka mpya

    (GMT+08:00) 2017-01-01 15:52:01


    Marafiki wapendwa,

    Katika wakati huu tunapouaga mwaka 2016 na kukaribisha mwaka mpya, ningependa kutoa salamu za mwaka mpya kwa wasikilizaji wetu popote mlipo duniani, kwa naiba ya Radio China Kimataifa na mimi binafsi, na kuwatakia furaha na kila la heri!

    Hivi karibuni, Radio China Kimataifa imeadhimisha miaka 75 tangu kuanzishwa kwake, wasikilizaji wengi wetu wa nchi za nje walitutumia salamu za pongezi. Msikilizaji wetu wa India aliandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii kuwa "Toka utangazaji wa masafa mafupi hadi tovuti ya habari kwenye mtandao wa Internet, hadi mitandao ya kijamii na APP kwenye simu za mkononi, Radio China Kimataifa imeambatana nasi wakati wote. Nawatakia CRI mafanikio makubwa zaidi na heri ya siku ya kuzaliwa!"

    Salamu ni fupi, lakini zinawakilisha maoni ya marafiki wengi, na pia imeonesha nyayo za CRI za kuendelea kupiga hatua mbele kuendana na wakati. Marafiki wapendwa, ni kutokana na uungaji mkono na ufuatuliaji wenu, hatua zetu za kuelekea mbele zimepata nguvu kubwa ya msukumo. Maendeleo ya Radio China kimataifa hayaondokani na uungaji mkono kutoka kwa wasikilizaji walioko nchi mbalimbali kote duniani, ningependa kutumia fursa hii kutoa shukrani zangu za dhati kwenu!

    Mwaka 2016, dunia imefikia kwenye hatua muhimu ya maendeleo, ambapo China inazidi kuonesha uwezo wake na kutoa mchango wake. Kwenye mkutano wa kilele wa G20 uliofanyika Hangzhou, China ilitoa busara zake maalumu kwenye usimamizi wa dunia, na pendekezo la Ukanda mmoja na Njia moja limeitikiwa na nchi nyingi zaidi. Kwenye jukwaa la kimataifa, China imeonesha sura ya nchi kubwa yenye kuwajibika.

    China iliyoko mbioni imeonesha ushawishi wake duniani, na maendeleo ya China yanafuatiliwa na dunia nzima. Radio China kimataifa inajitahidi kujenga daraja kati ya China na nchi za nje, ili kuifahamisha dunia kuhusu China. Katika mwaka uliopita, Radio yetu imeimarisha mageuzi na kuharakisha ushirikiano na vyombo vya habari vya nje, na kuwaelezea wasikilizaji wetu jinsi China ya leo ilivyo. Rais Xi Jinping wa China akiwa na viongozi wa Russia, Serbia na Bangladesh, walishuhudia kusainiwa kwa makubaliano ya ushirikiano kati ya CRI na vyombo vya habari vya nchi hizo. Mbali na hayo, pia hatusahau kufafanua ndoto zetu, ripoti kuhusu mkutano wa kilele wa G20 wa Hangzhou, urushaji wa maabara ya anga ya juu Tiangong No. 2 na chombo cha anga ya juu cha Shenzhou No. 11 zimefuatiliwa na kupendwa na wasikilizaji wetu. Tumejitahidi kuiunganisha China na dunia ya nje, kwa kuanzisha huduma mpya za habari kwa lugha mbalimbali kwenye simu za mkononi yaani China News, China Radio, na China TV, pia tumepanga kutoa APP zetu za simu ya mkononi za lugha ya Kiingereza, Kirusi, Kiitalia, Kijapani, Kihispania na Kihindi. Aidha tunajitahidi kuwasiliana na dunia ya nje, shughuli mbalimbali zikiwemo mahojiano ya wanahabari wa China na Russia kwenye njia ya hariri nchini China, Mkutano wa viongozi wa vyombo vya habari kwenye Baraza la Boao la Asia, Maonesho ya nyimbo kati ya China na ASEAN kwa mwaka 2016 na mazungumzo kati ya wanafunzi wa vyuo vikuu vya China na Marekani, zimepata ufuatiliaji mkubwa.

    Juhudi huzaa matunda. Mwaka 2016, tumepata mafanikio makubwa, kiasi cha jumla cha mawasiliano na wasikilizaji kimefikia milioni 55.3, idadi ya vilabu vya wasikilizaji imefikia 4,115, idadi ya jumla ya watumiaji wa huduma zetu imefikia milioni 260, na idadi ya wafuatiliaji kwenye mitandao ya kijamii imezidi milioni 80. Ninyi sio tu ni sehemu ya nambari hizi, bali pia ni marafiki zetu.

    Ndio ni kama msikilizaji wetu kutoka Bulgaria Valentina Nikolova alivyosema kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii kwamba "CRI inakupatia mabawa ya ndoto, inakuonyeshea mazuri ya China, na pia inakufahamisha kwa kina zaidi kuhusu nguvu ya urafiki! Shukrani kwa marafiki kutoka China!"

    Maneno hayo ni kama kutiwa moyo na rafiki wa muda mrefu, yanatukumbusha malengo yetu ya awali, na kutuhimiza tuendelee na juhudi kuelekea mafanikio ya ndoto yetu.

    Mwaka kesho ni mwaka wa kuku kwenye kalenda ya kilimo ya China. Kwa Radio China Kimataifa yenye historia ya miaka 75, mwaka mpya humaanisha mwanzo mpya. Tutaendelea na juhudi zetu za kuinua uwezo wa kupashana habari na kuendelea kuboresha huduma zetu, ili marafiki zetu waifahamu China zaidi, waielewe zaidi China, na waipende China zaidi!

    Napenda kutumia fursa hii kutoa salamu za heri ya mwaka mpya, Shukrani!

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako