• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • 39 wauawa kwenye shambulizi la kigaidi kwenye klabu ya usiku Istanbul

    (GMT+08:00) 2017-01-01 17:10:07

    Watu 39 wameuawa na wengine 69 wamejeruhiwa kwenye shambulizi la risasi lililotokea mapema ya leo asubuhi katika klabu maarufu ya usiku mjini Istanbul, Uturuki.

    Gavana wa Istanbul Vasip Sahin amesema shambulizi hili la kigaidi lilitekelezwa na mtu mwenye bunduki.

    Mchambulizi wa usalama aliyekataa jina lake kutajwa amesema mshambuliaji aliwaua walinzi wa usalama kabla ya kushambulia klabu hiyo, ambayo inaripotiwa kuwa kulikuwa na watu 400 waliosherehekea mwaka mpya. Amesema mtu huyu mwenye bunduki aliyevaa kama Baba Krismasi akiongea Kiarabu alibadilisha chemba za risasi mara nyingi katika shambulizi lake.

    Hatua za usalama zimeripotiwa kuimarishwa mjini Ankara na Istanbul kwa ajili ya sherehe za mwaka mpya, ikiwemo kuzuia kuingia kwa malori.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako