• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ligi kuu ya Uingereza imeendelea juzi na jana

    (GMT+08:00) 2017-01-02 08:30:17

    Liverpool imemaliza Mwaka 2016 kwa ushindi mtamu kwao Anfield walipoitungua Manchester City 1-0 na kubaki nafasi ya Pili kwenye ligi kuu ya Uingereza (EPL), wakiwa Pointi 6 nyuma ya Vinara Chelsea.

    Bao pekee na la ushindi kwenye Mechi hiyo lilifungwa Dakika ya 8 tu kwa Krosi ya Adam Lallana iliyounganishwa kwa Kichwa safi cha Georginio Wijnaldum.

    Mechi zingine za ligi hiyo ziliendelea jana jumapili ambapo, Arsenal wameanza vyema Mwaka Mpya 2017 kwa kuichapa Crystal Palace 2-0 huko Emirates na kukamata nafasi ya Tatu kwenye Ligi Kuu England EPL, Bao la kwanza la Arsenal lilifungwa na Olivier Giroud kwa Kisigino katika Dakika ya 17 na kudumu hadi Mapumziko.

    Dakika ya 56 Arsenal wakapiga Bao la Pili kupitia Alex Iwobi.

    Nayo Tottenham Hotspurs imeitandika Watford goli 4-1, Harry Kane na Dele Alli alipiga Bao 2 kila mmoja. Ligi hiyo ya EPL itaendelea tena leo kwa Mechi 6.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako