• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Asilimia 46 tu ya Wamarekani wanaamini uwezo wa Donald Trump kutatua msukosuko wa kimataifa

    (GMT+08:00) 2017-01-03 19:11:29

    Utafiti wa maoni ya watu nchini Marekani uliofanywa na Kampuni ya Gallup umeonesha kuwa, ni asilimia 46 tu ya watu waliohojiwa ambao wanaamini kuwa rais mteule wa Marekani Donald Trump anaweza kutatua msukosuko wa kimataifa.

    Utafiti huo pia umesema, asilimia 47 waamini kuwa atatumia kwa busara nguvu za kijeshi huku asilimia 44 wakiona kuwa anaweza kuzuia kashfa kubwa kutokea kwenye serikali yake.

    Hata hivyo wamarekani wameeleza imani yao na Trump katika kushirikiana kwa ufanisi na bunge, ikiwa ni asilimia 60, kushughulikia vizuri uchumi, asilimia 59, kulinda maslahi ya Marekani nje ya nchi akiwa rais, askilimia 55 na kuweza kusimamia ofisi ya ikulu ya Marekani asilimia 53.

    Habari nyingine zinasema, msemaji wa Bw. Trump Sean Spicer amesema, hakuna ushahidi unaothibitisha kuwa Russia imeshambulia na kuathiri uchaguzi wa Marekani uliofanyika mwaka jana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako