• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkuu wa WildAid apongeza uamuzi wa China wa kupiga marufuku kabisa biashara ya pembe za ndovu

    (GMT+08:00) 2017-01-03 19:43:24

    China itasimamisha hatua kwa hatua usindikaji na mauzo ya pembe za ndovu kwa ajili ya malengo ya kibiashara kabla ya mwisho wa mwaka huu, ikiwa ni hatua nyingine zaidi ya kupambana na biashara haramu ya wanyama na mimea pori.

    Akizungumzia uamuzi huu wa serikali ya China, mwanzilishi mwenza na mkurugenzi mtendaji wa Shirika la kimataifa la wanyamapori la WildAid Peter Knights amesema utasaidia kupunguza ujangili barani Afrika, kwani biashara ya pembe za ndovu ikisimamishwa, bei ya pembe hizo itakabiliwa na shinikizo kubwa. Pia ametoa mwito kwa nchi nyingine kufuata nyayo za China na kupiga marufuku kikamilifu biashara ya pembe za ndovu, ili kuwalinda vizuri wanyama pori.

    Kwa mujibu wa Mamlaka ya Misitu ya Taifa ya China, hatua hiyo itaathiri makampuni 34 ya usindikaji na maeneo 143 yaliyoteuliwa kuuza pembe za ndovu, na kwamba makumi kati yao yatafungwa kabla ya mwisho wa mwezi Machi mwaka huu na yatakayobaki yatafungwa kabla ya mwisho wa mwaka huu.

    Kabla ya muda wa kikomo, mashirika ya utekelezaji sheria yataendelea kupambana na vitendo haramu vinavyohusiana na pembe za ndovu.

    Wakati huohuo, mwenyekiti wa Shirika la Huduma kwa Wanyapori nchini Kenya KWS Richard Leakey amepongeza uamuzi wa serikali ya China, na kusema utaleta nguvu mpya kwa dunia katika mapambano dhidi ya biashara haramu ya pembe za ndovu. Amesema kizuizi kilichowekwa na China dhidi ya bidhaa za pembe za ndovu kimeichochea jamii ya kimataifa kuongeza juhudi katika kusimamisha vifo vya Tembo wa Afrika vinavyotokana na ujangili na hali mbaya ya hewa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako