• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wafungwa 158 watoroka baada ya jela moja kusini mwa Philippines kushambuliwa

    (GMT+08:00) 2017-01-04 19:01:14

    Serikali ya Philippines imethibitisha kuwa, wafungwa 158 wametoroka baada ya gereza moja kusini mwa nchi hiyo kushambuliwa.

    Afisa wa gereza hilo Bw. Peter Bongat amesema, watu zaidi ya 100 waliokuwa na silaha mapema leo asubuhi walishambulia gereza moja lililoko jimbo la North Cotabato kwa kutumia silaha nzito. Bw. Bongat amesema huenda watu hao wanatoka kundi la upinzani la Bangsamoro Islamic Freedom Fighters.

    Kikosi maalum cha polisi kinawasaka wafungwa hao waliotoroka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako