• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan na China kuendeleza ushirikiano kwenye sekta ya madini

    (GMT+08:00) 2017-01-04 19:41:31

    Serikali ya Sudan imeahidi kutoa mazingira yanayofaa kwa wawekezaji kutoka China watakaowekeza kwenye sekta ya uchimbaji madini nchini humo, pamoja na kutoa ulinzi unaotakiwa kwa wachimbaji kutoka China.

    Waziri wa madini wa Sudan Ahmed Mohamed Sadiq Al-Karuri amesema, nchi yake ina mazingira mazuri kwa uwekezaji yanayovutia wawekezaji kutoka nchi mbalimbali.

    Balozi wa China nchini Sudan Li Lianhe amesema, China imeweka umuhimu mkubwa katika ushirikiano na Sudan katika sekta ya uchimbaji madini. Ameongeza kuwa, China tayari imepeleka wataalam wengi wa fani hiyo nchini Sudan ili kuimarisha ushirikiano kati ya pande hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako