• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yataka kusimamishwa kwa mchakato wa kuweka Thaad

    (GMT+08:00) 2017-01-05 19:45:18

    Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Geng Shuang amesema China inazitaka pande husika zisimamisha mchakato wa kuweka mfumo wa ulinzi dhidi ya makombora THAAD, na inapenda kushauriana na Korea Kusini ili kupata ufumbuzi mwafaka kwenye msingi wa kuangalia maslahi ya kila upande.

    Bw. Geng amesema China imeeleza ufuatiliaji na pingamizi zake kuhusu mfumo huo, na kwamba Marekani kuweka mfumo wa Thaad nchini Korea Kusini kutaharibu uwiano wa mkakati wa kanda hiyo, kuharibu maslahi ya usalama wa kimkakati wa China na pia hakusaidii amani na utulivu kwenye Peninsula ya Korea.

    Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi jana hapa Beijing alikutana na ujumbe wa Chama cha Minjoo cha Korea Kusini, ambapo pande hizo mbili zilibadilishana maoni kuhusu suala la Thaad.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako