• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uzoefu wa utalii wahimiza mawasiliano kati ya watu wa China na Afrika

    (GMT+08:00) 2017-01-05 19:53:39

    Kuanzia tareh 7 hadi 12, waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi atafanya ziara katika nchi tano barani Afrika. Miaka 27 iliyopita, Afrika ilikuwa kituo cha kwanza cha ziara iliyofanywa na waziri wa mambo ya nje wa China baada ya mwaka mpya. Msingi wa uhusiano kati ya pande hizo mbili upo kwenye mawasiliano baina ya watu wao, na kadiri ushirikiano kati ya China na Afrika unavyoendelea, ndivyo watu wa pande hizo mbili wanavyoaminana zaidi, na hadithi nyingi za watu wa kawaida zinatueleza kuwa, wapo wafrika wengi wanaofuata ndoto zao nchini China, huku vilevile kuna wachina wengi wanaojiendeleza katika nchi za Afrika. Moja ya njia ya ushirikiano kati ya China na Afrika, ni taasisi moja hapa nchini China, ambayo inashughulikia kuandaa shughuli za utalii barani Afrika iitwayo "Bobu Afrika". Mwanzilishi wa taasisi hii ni Shi Yingying. Neno "Bobu" linatokana na tamko la Kiingereza la mti wa Baobab, kwa Kiswahili ni Mbuyu, ukiwa na maana ya kuweka mizizi kwenye ardhi ya Afrika, kueneza uzuri na maajabu wa bara hilo, ili watu wengi zaidi nchini China waweze kupewa zawadi bora zaidi kutoka Afrika.

    Wakati "Bobu Afrika" inaanza, Wachina wanaopenda kupiga picha waliwaonesha wenzao picha za mandhari, wakazi na utamaduni walizopiga barani Afrika, picha hizo vilevile zilirekodi michango iliyotolewa na Wachina kwa ajili ya maendeleo ya Afrika.

    Siku baada ya siku "Bobu Afrika" ilianza kutoa huduma ya utalii kwa Wachina toka kupata uzoefu wa utalii kwa kupiga picha hadi kulinda wanyamapori na kutunza jamii. Ili kueneza zaidi utamaduni wa China barani Afrika na ule wa Afrika hapa China, njia nzuri ni kupitia bidhaa.

    Tangu kupiga picha barani Afrika hadi kujulisha bidhaa za Afrika, mpaka sasa kujumuisha kupata uzefu wa utalii, "Bobu Afrika" inabadilika na kujiendeleza, na kukua kutoka shirikisho moja la kujitolea lenye matumaini madogo hadi kuwa jukwaa la njia ya kisasa ya mawasiliano inayowajibika na kuwaunganisha watu China na watu wa Afrika. Kutokana na ufahamu na heshimu kwa utamaduni wao wenyewe na utamaduni wa Afrika wa kipekee, Bobu hutoa mafunzo na mwongozo kwa watalii watakaosafiri Afrika kuhusu mambo yanayotakiwa kufahamiwa na kuzingatiwa katika mawasiliano na watu wa huko.

    Bobu Afrika ilianzisha mradi uitwao "Kama huwezi kwenda Afrika, basi nakuonesha Afrika kwako." mradi unaolingana na ule "Kama huwezi kutembelea China basi tukuonesha kwako" Watu wengi waliosafiri Afrika walitembea vituo vya kuwatunza wazee ama watoto, na kuwaelezea hadhiti zao za safari barani Afrika.

    Hivi sasa Bobu Afrika ni moja tu ya jukwaa la mawasiliano ya kisasa nchini China zinazotoa huduma za utalii barani Afrika, ambazo zinachangia katika kusukuma mbele mawasiliano ya watu wa China na Afrika kwa hatua zao halisi zenye ufanisi na nguvu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako