• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuongeza uwekezaji kwenye sekta ya nishati endelevu

    (GMT+08:00) 2017-01-06 19:02:16

    China itaongeza uwekezaji wa dola za Marekani bilioni 361 kwenye sekta ya nishati endelevu katika miaka mitano ijayo na kuifanya nishati hiyo kuwa chanzo kikuu cha ongezeko la nishati na nguvu ya umeme nchini China.

    Naibu mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Nishati ya China Bw. Li Yangzhe amesema, inatarajiwa kuwa matumizi ya nishati isiyo ya kisukuku yatafikia asilimia 15 ifikapo mwaka 2020, na asilimia 20 mwaka 2030. Pia amesema kipaumbele kitawekwa katika kuhimiza matumizi ya vyombo vya usafiri vinavyotumia nishati safi, gharama ndogo za nishati endelevu kama vile upepo, kuongeza ufanisi wa matumizi ya nishati na kuongeza ubunifu na ushirikiano wa uzalishaji wa kimataifa kwenye sekta ya nishati.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako