Washindi wa mbio za mwaka huu za dunia kwa wachezaji mmoja mmoja atapata dola za Marekani 30,000. Huku washindi wa pili kwa wanaume na wanawake kila mmoja ataondoka na dola 3,000.
Kwa upande wa zawadi za kitimu, timu itakayoshinda itatwaa dola za Marekani 20,000 wakati ile ya pili itaondoka na dola 16,000 na hadi mshindi wa sita atapata zawadi. Washindi wa mbio za kupokezana vijiti wataondoka na kitita cha dola za Marekani 12, 000.
Tayari Shirikisho la Riadha la Uganda (UAF) limetangaza kikosi cha wachezaji 49 akiwemo bingwa wa marathoni wa Olimpiki Stephen Kiprotich.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |