• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China atoa tuzo ya ngazi ya juu ya kisayansi kwa Tu Youyou

    (GMT+08:00) 2017-01-09 18:35:14

    Kamati kuu ya Chama cha kikomunisti cha China na Baraza la mawaziri la China leo asubuhi wameandaa Mkutano wa utoaji wa tuzo za kisayansi za taifa katika Jumba la mikutano ya umma mjini Beijing, ambapo viongozi wakuu wa chama na serikali akiwemo Rais Xi Jinping, Waziri Mkuu Bw Li Keqiang, Bw Liu Yunshan, na Bw Zhang Gaoli wameshiriki.

    Wanasanyansi wawili wa China wakiwemo mwanasayansi wa fizikia Zhao Zhongxian na mwingine wa dawa Bibi Tu Youyou wameshinda tuzo ya ngazi ya juu ya sayansi ya taifa, kutokana na michango yao kwa uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia. Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang alipotoa hotuba kwa niaba ya kamati kuu ya chama na baraza la serikali amesema :

    "Hivi sasa duru mpya ya mapinduzi ya kisayansi na mageuzi ya viwanda imefanyika duniani, huku marekebisho ya kimuundo ya uchumi pia yakiingia katika kipindi kipya, ni lazima kutoa kipaumbele kwa uvumbuzi katika sehemu ya muhimu ya maendeleo ya China, kufuata kanuni mpya ya maendeleo, kufanya mageuzi ya kimuundo na kukuza mkakati wa kufanya uvumbuzi, ili kuhimiza uchumi kupata ongezeko la kasi."

    Bw. Li Keqiang pia anasisitiza kuwa, China inapaswa kuongeza uwezo wa kufanya uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia, ili kuhakikisha uwezo wa ushindani wa taifa. Anasema:

    "Inapaswa kuhimiza mageuzi ya mfumo wa sayansi na teknolojia, kuipa taasisi ya sayansi na utafiti pamoja na vyuo vikuu madaraka makubwa zaidi ya kujiamulia, kuwapa wanasayansi wanaofanya uvumbuzi haki haki kubwa zaidi ya kutumia raslimali watu na vitu, na kuhimiza utekelezaji wa sera za utoaji wa faida kwa wanasayansi hao, ili kufanya watu hao wapewe heshima na sifa wanaostahili."

    Bw. Li Keqiang pia amesisitiza kuwa inatakiwa kuhimiza matokeo ya uvumbuzi kutumika katika sekta mbalimbali, ili kuingiza nguvu ya uhai katika sekta za jadi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako