• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ronaldo ashinda tuzo ya mwanasoka bora wa FIFA, Ranieli achukua tuzo ya kocha bora

    (GMT+08:00) 2017-01-10 09:30:14

    Mshambuliaji Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) mwaka 2016 baada ya kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya na Real Madrid na kuiwezesha Ureno kutwaa Kombe la Euro.

    Nyota huyo mwenye umri wa miaka 31 kwa mara nyingine amemuangusha mpinzani wake, Lionel Messi kama alivyofanya awali mwezi uliopita kwenye Ballon d'Or.

    Naye Kocha wa Mabingwa wa England, Leicester City, Claudio Ranieri amebeba tuzo ya Kocha Bora duniani. Ranieri raia wa Italia aliiwezesha Leicester kubeba ubingwa wa England msimu uliopita na kuushangaza ulimwengu. Huku Kocha wa zamani wa timu ya Taifa ya Ujerumani kwa wanawake, Silvia Neid amebeba tuzo ya kocha bora wa dunia upande wa wanawake huku Mohamed Faiz Subri akitwaa tuzo ya goli bora ya Puskas kwa 2016.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako