• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa Tanzania akutana na waziri wa mambo ya nje wa China

    (GMT+08:00) 2017-01-10 12:32:19

    Waziri mkuu wa Tanzania Bw. Kassim Majaliwa amekutana na waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi mjini Dar es Salaam, Tanzania.

    Kwenye mazungumzo yao Bw. Majaliwa amesema Tanzania inaishukuru China kwa kuichagua Tanzania kuwa moja ya nchi nne za Afrika katika ushirikiano wa kuhimiza uwezo wa uzalishaji viwandani, na inapenda makampuni mengi zaidi ya China yashiriki kwenye miradi ya ujenzi nchini humo.

    Kwa upande wake Bw. Wang Yi ametaka nchi hizo mbili ziendeleze ushirikiano wa kiuchumi na kiutamaduni, kuzidisha mawasiliano ya kijeshi na kuimarisha uratibu kwenye mambo ya kimataifa, ili kuwanufaisha zaidi watu wa Tanzania.

    Wakati huo huo, Bw Wang Yi pia amefanya mazungumzo na mwenzake wa Tanzania Bw Augustine Mahiga.

    Bw Mahiga amesema Tanzania inapenda kupanua ushirikiano na kuzidisha uhusiano wa kiwenzi na China, ili kuhimiza maendeleo ya uchumi wa Tanzania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako