• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Cleveland Cavaliers waibuka washindi NBA

    (GMT+08:00) 2017-01-11 08:38:04

    Ligi ya kulipwa ya mpira wa kikapu ya NBA nchini Marekani, mabingwa watetezi Cleveland Cavaliers wameibuka na ushindi wa alama 116 dhidi ya 108 za Brooklyn Nets.

    Katika mchezo huo, nyota wa Cleveland, Lebron James alifunga alama 36 peke yake. Kyrie Irving nae akaipa chagizo la ushindi Cleveland kwa kufunga alama 32.

    Katika matokeo mengine Houston Rockets wamewanyuka Orlando Magic alama 100 kwa 93 huku mchezaji wao nyota James Harden akifunga alama 14 na kutoa pasi 10 za ushindi.

    Nao Memphis Grizzlies wamewatoa nishai Golden State Warriors kwa kuwapa kipigo cha alama 128 kwa 119, Miami Heat wakinyukwa alama 127 kwa 100 dhidi ya Los Angeles Lakers mechi nyingine ilikuwa kati ya Boston Celtic wameshinda kwa alama 110 kwa 106 dhidi ya Philadelphia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako