• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa mwaka wa baraza la uchumi la dunia kusisitiza uongozi mpya wa kimataifa

    (GMT+08:00) 2017-01-11 19:19:39

    Mwanzilishi wa baraza la uchumi la dunia ambaye pia ni mwenyekiti mtendaji wa baraza hilo Bw. Klaus Schwab amesema dunia inahitaji uongozi mpya utakaofuata hali halisi na kuwajibika zaidi.

    Bw.Schwab amesema, dunia inakabiliana na mabadiliko na maendeleo ya kasi, na uongozi mpya unahitajika ambao utatilia maanani mustakabali, na kuwa na lengo wazi, na kufanya juhudi kwa pamoja ili kutatua changamoto zilizopo.

    Wakati huohuo, Rais Xi Jinping wa China atafanya ziara nchini Uswis kuanzia tarehe 15 hadi 18 mwezi huu, ambapo atahudhuria mkutano wa mwaka 2017 wa baraza la uchumi duniani utakaofanyika huko Davos. Naibu waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Li Baodong leo amesema, hii ni mara ya kwanza kwa rais Xi Jinping kuhudhuria mkutano huo. Amesema:

    "Rais Xi Jinping ataeleza maoni ya China kuhusu masuala ya utandawazi wa kiuchumi yanayofuatiliwa na jumuiya ya kimataifa, kuhimiza pande mbalimbali kutambua na kufuata utandawazi wa kiuchumi, na kuongoza mchakato wa utandawazi wa uchumi uwe na masikilizano na manufaa kwa watu wote. Kuchambua kwa undani chanzo cha matatizo yanayozuia ongezeko la uchumi duniani, na kutafuta njia ya kutatua matatizo hayo. Kueleza mafanikio na uzoefu wa maendeleo ya kufungua mlango ya China, na kuongeza ufahamu wa pande mbalimbali kwa uchumi wa China. "

    Amesema China inapenda kujadiliana na pande mbalimbali kuhusu kukabiliana changamoto kubwa duniani na kuhimiza maendeleo yenye afya na utulivu ya uchumi duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako