• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yapokea vichwa sita vya treni kutoka China

    (GMT+08:00) 2017-01-12 09:42:13

    Kenya imepokea vichwa sita vya treni kutoka China, ambavyo vitatumika kwenye reli ya SGR iliyojengwa kwa ufadhili wa serikali ya China inayotarajiwa kuanza kutoa huduma mwezi Juni mwaka huu.

    Akiongea kwenye hafla ya kupokea vichwa hivyo kwenye kituo cha treni mjini Mombasa, waziri wa uchukuzi na miundombinu wa Kenya Bw. James Macharia amesema kukabidhiwa kwa sehemu ya kwanza ya vichwa vya treni kutoka China ni hatua muhimu kwenye mchakato wa kukamilisha mradi wa reli ya SGR kati ya Mombasa na Nairobi.

    Reli hiyo yenye urefu wa kilomita 472 inayounganisha miji hiyo miwili imejengwa na kampuni ya China CRBC, na Kenya itapata vichwa 56 vya treni kutoka China ili kusafirisha abiria na mizigo kwenye reli hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako