• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Barcelona yasema mkataba mpya wenye nyongeza wa Lionel Messi utategemea mapato ya wadhamini na uuzaji wa wachezaji

    (GMT+08:00) 2017-01-12 09:58:02

    Mkurugenzi mkuu wa klabu ya Barcelona Oscar Grau amesema mpango wa klabu hiyo kumpatia Lionel Messi mkataba mpya wenye nyongeza ya mshahara utategemea uwezo wao wa kuvutia mapato kutoka kwa wadhamini na uuzaji wa wachezaji.

    Mkataba wa Messi unakamilika 2018 na anatarajia kupewa mkataba mpya huku ikiripotiwa huenda akapewa kitita cha pauni milioni 21 wanazopata Luis Suarez na Neymar.

    La Liga huweka mkataba na kila klabu kuhusu matumizi yao kila mwanzo wa msimu, ambapo huzizuia bodi kutotumia zaidi ya asilimia 70 ya bajeti yake ya mapato. Mkataba wenye mishahara mikubwa waliyopatiwa Suarez na Neymar ambayo itakamilika 2021, huchukua kiwango kikubwa cha matumizi ya timu hiyo.

    Messi mwenye umri wa miaka 29, anaripotiwa kupokea pauni milioni 19 na Grau anasema kuwa nyongeza yoyote lazima ifikiriwe sana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako