• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Dimitri Payet hataki tena kuichezea West Ham

    (GMT+08:00) 2017-01-13 08:57:35

    Mkufunzi wa klabu ya West Ham Slaven Bilic amesema mshambuliaji Dimitri Payet hataki tena kuichezea West Ham, lakini klabu hiyo haiko tayari kumuuza.

    Raia huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 29 amekuwa akihusishwa na swala la kuihama timu hiyo. Payet alijiunga na West Ham kutoka Merseille kwa kitita cha pauni milioni 10.7 mnamo mwezi Juni 2015. Alifanikiwa katika msimu wa kwanza na klabu hiyo, akifunga mabao 12.

    Ijapokuwa amefunga mara tano msimu huu, Payet ameshindwa kufikia kiwango kama hicho na kwa mujibu wa ripoti Bilic alimuagiza mchezaji huyo kubadili tabia yake.

    Aliwachwa nje katika mechi ya FA siku ya Ijumaa ambapo West Ham ililazwa 5-0 na Manchester City.

    West Ham iko nafasi ya 13 katika ligi ya Uingereza, alama saba juu ya eneo la kushushwa daraja na sasa itakwaruzana na Crystal Palace siku ya Jumamosi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako