• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani yatangaza kufuta sera maalumu ya uhamiaji kwa wazamiaji kutoka Cuba

    (GMT+08:00) 2017-01-13 18:12:42

    Rais Barack Obama wa Marekani amesema, Marekani itafuta mara moja sera maalumu ya uhamiaji kwa wazamiaji kutoka Cuba ili kuhimiza mchakato wa kuufanya uhusiano kati ya nchi hizo mbili uwe kawaida.

    Rais Obama amesema, wizara ya usalama wa ndani ya Marekani itafuta sera hiyo iliyotekelezwa kwa miaka zaidi ya 20, na kwamba raia wa Cuba wanaojaribu kuingia Marekani kwa njia haramu zisizoambatana na masharti ya msaada wa kibinadamu, watarejeshwa nyumbani kama raia wa nchi nyingine. Rais Obama amesema serikali ya Cuba imekubali kupokea raia wake waliorejeshwa na Marekani.

    Serikali ya Cuba jana imesema, kufutwa kwa sera hiyo ni hatua muhimu ya kuhimiza uhusiano kati ya nchi hizo mbili uwe kawaida.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako