• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Msimu wa safari nyingi zaidi duniani waanza

    (GMT+08:00) 2017-01-13 18:32:10

    Msimu wa safari nyingi zaidi duniani umeanza nchini China hii leo, huku idadi kubwa ya safari ikitarajiwa kuongezeka wakati wa sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa Kichina.

    Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa Kichina ni sikukuu muhimu kwa familia za Kichina, ambapo mamilioni ya watu wanarejea kwenye maskani zao kuunganika tena na ndugu na jamaa, hivyo kuweka shinikizo kubwa katika mfumo wa usafiri.

    Wizara ya uchukuzi ya China imesema, jumla ya safari bilioni 2.978 zinatarajiwa wakati wa msimu huu wa sikukuu, ikiwa ni ongezeko la asilimia 2.2 ikilinganishwa na mwaka jana kipindi kama hicho. Wizara hiyo imesema safari za treni zitaongezeka zaidi wakati wa sikukuu ili kukabiliana na idadi kubwa ya wasafiri, na utaratibu wa mauzo ya tiketi utarahisishwa zaidi ili kuboresha huduma hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako