• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • ECOWAS yashindwa kumshawishi rais wa Gambia kuachia madaraka

    (GMT+08:00) 2017-01-14 20:18:32

    Ujumbe wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Magharibi ya Afrika ECOWAS ulioongozwa na waziri wa mambo ya nje wa Nigeria Geoffrey Onyeama umeshindwa kufikia makubaliano na rais wa Gambia Yaya Jammeh ya kuachia madaraka. Hata hivyo Bw. Onyeama amesema matokeo hayo sio ya mwisho.

    Ujumbe uliokwenda Banjul ulijumuisha rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf, ambaye pia ni mwenyekiti wa ECOWAS na rais wa zamani wa Ghana John Mahama. Na walikuwa na mkutano wa faragha na rais Jammeh, na baadaye kukutana na rais mteule Adama Barrow. Kwa mujibu wa Onyeama ujumbe huo utawaarifu wakuu wa nchi juu ya mazungumzo yao na baadaye wakuu hao kutoa uamuzi yakinifu juu ya mpango wa utekelezaji.

    Jammeh alishindwa kwenye uchaguzi wa rais wa Disemba mosi ambapo awali alikubali matokeo lakini baadaye akabadili mawazo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako