• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan yatarajia uhusiano wa kawaida na Marekani

    (GMT+08:00) 2017-01-15 17:10:34

    Waziri wa mambo ya nje wa Sudan Ibrahim Ghandour amesema nchi yake inatarajia uhusiano wa kawaida kati ya Sudan na Marekani baada ya kuondolewa kwa baadhi ya vikwazo vya kiuchumi ilivyowekewa.

    Akiongea na wanahabari Bw. Ghandour amesema uamuzi huo umekuja baada ya majadiliano ya kina yaliyodumu kwa miaka miwili. Amesisitiza kuwa nchi yake imedhamiria kushirikiana kwa kina na serikali ya Marekani na inategemea Marekani nayo itadhamiria pia.

    Hata hivyo, serikali ya Sudan imesema kuondolewa kwa baadhi ya vikwazo ni haki ya kawaida ya nchi yake, na sio zawadi. Rais wa Sudan Omar al-Bashir ameelezea uamuzi huo kuwa ni maendeleo makubwa na kwamba umekuja wakati ambao Sudan inakamilisha mchakato wa majadiliano ya kitaifa na kuendelea mbele na uundaji wa serikali ya maridhiano ya kitaifa.

    Wakati huohuo Umoja wa Mataifa nao umepongeza uamuzi huo wa Marekani na kusema umetambua hatua zinazochukuliwa na serikali ya Sudan katika miezi ya karibuni kwenye maeneo mengi muhimu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako