• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaiambia Marekani kuwa sera ya China moja haitakiwi kujadiliwa

    (GMT+08:00) 2017-01-15 17:23:20

    China imeiambia Marekani kuwa sera ya China moja ni msingi wa kisiasa wa uhusiano kati yao na haitakiwi kujadiliwa.

    Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Lu Kang ameyasema hayo akijibu kauli iliyotolewa na rais mteule wa Marekani Donald Trump kuwa sera ya China moja kuhusu Taiwan inaweza kujadiliwa na kwamba yeye haahidi kuifuata kikamilifu. Trump amenukuliwa akisema Ijumaa kwenye mahojiano na Jarida la Wall Street Journal kuwa kila kitu kiko kwenye mazungumzo ikiwemo sera ya China moja.

    Bw. Lu amesema ni lazima kubaini kuwa kuna China moja tu duniani na Taiwan ni sehemu isiyotengwa ya China. Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China ni serikali pekee halali inayoiwakilisha China, ukweli ambao unatambuliwa kimataifa na hakuna mtu anayeweza kuubadilisha.

    Ameongeza kuwa China inataka pande husika nchini Marekani kutambua unyeti mkubwa wa suala la Taiwan na kufuata ahadi zilizotolewa na awamu zilizopita za serikali za Marekani kuhusu sera ya China moja na kanuni za taarifa tatu za pamoja. Lu ameihimiza Marekani kushughulikia kwa mwafaka suala la Taiwan ili kuepusha kuharibu maendeleo mazuri na yenye utulivu kati ya China na Marekani na ushirikiano katika maeneo muhimu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako