• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China aanza ziara rasmi nchini Uswisi

    (GMT+08:00) 2017-01-16 10:15:08

    Rais Xi Jinping wa China ameanza ziara nchini Uswisi na kusema China inatarajia kuimarisha urafiki na kukuza ushirikiano kati yake na Uswisi. Rais amesema hayo kwenye sherehe ya kumkaribisha iliyoandaliwa na wajumbe saba wa Baraza la serikali la nchi hiyo.

    Rais Xi amewasili mjini Zurich jana adhuhuri na kuanza ziara yake rasmi ya siku nne nchini Uswisi, ikiwa ni ziara ya kwanza ya rais wa China nchini humo katika karne ya 21.

    Kwenye ziara hiyo, rais Xi anatarajiwa kuhudhuria mkutano wa mwaka 2017 wa Baraza la uchumi duniani WEF utakaofanyika huko Davos, na kutembelea makao makuu ya ofisi ya Umoja wa Mataifa na Shirika la afya duniani mjini Geneva, na makao makuu ya Kamati ya Olimpiki ya kimataifa yaliyoko mjini Lausanne.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako