• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 32 wafariki baada ya ndege ya kubeba mizigo ya Uturuki kuanguka nchini Kyrgyzstan

    (GMT+08:00) 2017-01-16 17:05:16

    Watu 32 wamefariki dunia baada ya ndege ya kubeba mizigo ya Uturuki kuanguka mapema leo karibu na uwanja wa ndege wa Bishkek-Manas, nchini Kyrgyzstan.
    Ndege hiyo aina ya Boeing 747 iliyokuwa ikielekea Istanbul kutoka Hongkong ilitarajiwa kutua kwenye uwanja huo wa ndege saa moja na dakika 20 leo kwa saa za huko, lakini ilianguka saa moja na nusu kwenye kijiji kimoja chenye watu wengi katika jimbo la Chu Oblast.
    Hivi sasa uwanja huo umefungwa, na chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako