• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • AFCON 2017

    (GMT+08:00) 2017-01-17 08:49:33

    Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo (DRC) IMEITWANGA Morocco na kuandika ushindi wa kwanza katika michuano ya AFCON 2017 inayoendelea nchini Gabon.

    ushindi huo umepatikana kupitia bao la Junior Kabananga aliyefunga katika dakika ya 55. Hata hivyo, Morocco ndiyo waliokuwa wakishambulia zaidi kuliko DR Congo waliokuwa makini katika kujilinda.

    DR Congo walipata pengo baada ya Lomalisa Mutambala aliyeingia katika dakika ya 64 kulambwa kadi ya pili ya njano na kuwa nyekundu katika dakika ya 85.

    Kipa Matambi ambaye ni kipa wa TP Mazembe, alikuwa kikwazo kikubwa kwa Morocco ambao walishambulia zaidi.

    Kwa ushindi huo, DR Congo sasa wanaongoza kundi C wakiwa na pointi tatu na kufuatiwa na Ivory Coast, Togo ambao kila mmoja ana pointi moja huku Morocco akiwa anaburuza mkia akiwa hana kitu.

    Katika mchezo mwingine Ivory Coast imetoka sare ya 0-0 na Togo huko Stade De Franceville mjini Franceville.

    Michuano hiyo inaendelea leo ambapo timu za kundi D zitacheza. Ghana itacheza dhidi ya Uganda, timu pekee toka Afrika Mahsariki. Na Mali itacheza na Egypt.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako