• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais wa China na Uswisi wakutana na wajumbe wa sekta za uchumi za Uswisi

    (GMT+08:00) 2017-01-17 14:16:35

    Rais Xi Jinping wa China anaendelea na ziara yake nchini Uswisi, jana pamoja na mwenzake wa Uswisi Bibi Doris Leuthard mjini Bern walikutana na wajumbe wa sekta za uchumi za Uswisi.

    Rais Xi amepongeza mafanikio yaliyopatikana kwenye ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Uswisi katika miaka 67 iliyopita tangu nchi hizo mbili zianzishe uhusiano wa kibalozi, na kusema pande mbili zina maslahi ya pamoja katika kulinda utaratibu ulio wazi na huru wa kiuchumi wa kimataifa, na anatumai kuwa nchi hizo mbili zitafanya juhudi kuendeleza ushirikiano wa kunufaishana.

    Rais Leuthard amesema China imekuwa mwenzi mkubwa wa kibiashara wa Uswisi barani Asia, na kusisitiza kuwa Uswisi ni moja ya nchi za magharibi zilizotambua mapema hadhi kamili ya China ya kuwa na uchumi wa soko huria, na ingependa kushirikiana na China katika kupanua ushirikiano wa kiuchumi kati yao.

    Siku hiyo rais Xi pia alikutana na maspika wa mabaraza mawili ya bunge la Uswisi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako