• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kombe la FA kuendelea leo, Liverpool ugenini

    (GMT+08:00) 2017-01-18 09:38:45

    Wakati Droo ya Raundi ya 4 ya Kombe kongwe Duniani, FA CUP, imeshafanyika, Leo Jumatano zipo Mechi za Marudiano za Raundi ya 3 kwa zile Timu zilizoenda Sare.

    Moja ya Timu hizo ni Vigogo Liverpool ambao walibanwa na Timu ya Daraja la chini Plymouth Argyle huko Anfield na kutoka 0-0 na sasa wanapaswa kwenda Ugenini kwa Timu hiyo ya Daraja la 4 ili kurudiana nao.

    Mshindi wa Mechi hiyo atakuwa Nyumbani kucheza Mechi ya Raundi ya 4 na Wolverhampton Wanderers. Mechi za Raundi ya 4 ya FA CUP zitaanza Ijumaa Januari 27 kwa Mechi 1 tu kati ya Derby County na Mabingwa wa England Leicester City. Mabingwa Watetezi wa FA CUP, Manchester United wao watacheza Raundi ya 4 kwao Old Trafford na Wigan Athletic hapo Jumapili Januari 29.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako