• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Polisi waongezewa magari 500 Kenya

    (GMT+08:00) 2017-01-18 16:19:04

    Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amezindua awamu ya tatu ya utoaji wa magari kwa idara ya polisi ambapo amekabidhi kikosi hicho zaidi ya magari mia tano.

    Magari hayo ni pamoja na yale ya kivita na ya usafirishaji wa maafisa wa polisi na yanatarajiwa kuboresha usalama nchini humo.

    Ronald Mutie anaripoti.

    Rais Uhuru Kenyatta akiwa kwenye bustani ya Uhuru anajaribu gari maalum la polisi lenye bunduki.

    Ni sehemu ya zaidi ya magari 500 ambayo serikali imekondisha ili kuimarisha usalama nchini Kenya.

    Bwana Joseph Boinet ni Inspeka jenerali wa polisi.

    "Tumezindua magari madogo 50, malori mia moja na lori ndogo 350 na pia magari maalum yaani m-raps 25"

    Magari hayo 25 kutoka China yana uwezo wa kuhimili risasi mabomu ya kutegwa ardhini.

    Yana uwezo wa kukimbia kwa kilomita 140 kwa saa yakibeba polisi 10 kwa safari moja, anasema waziri wa usalama Joseph Nkaiserry.

    "Baadhi ya magari tayari yamepelekwa kufanya oparesheni Baadhi yatapelekwa katika msitu wa Boni na mengine eneo la kaskazini mashariki nah ii ni sehemu tu ya mpango wetu wa kuboresha idara ya polisi ambao unaendelea"

    Maafisa wa polisi ambao watayatumia magari haya maalum pia wamepewa sare zenye kamera zilizo na uwezo wa kuona usiku.

    Kufuatia kuongezewa kwa magari haya sasa huduma ya polisi nchini Kenya ina magari 8,575 ikilinganishwa na 3,155 mwaka 2013.

    Pia ili kuimarisha usalama na doria angani idara ya huduma za polisi imepewa helikopta tatu na serikali inatarajia kuongezea hadi saba.

    Vifaa vyote hivi vinaendelea kuongezewa huku Kenya ikipata ufanisi katika vita dhidi ya ugaidi.

    Rais Uhuru Kenyatta anasema "Ili kupambana vilivyo na aina yoyote ile ya uhalifu ikiwemo ugaidi tunatambua kwamba polisi wetu wanahitaji vifaa maalum. Mwaka wa 2013 vifaa vyote maalum vya polisi vilikuwa katika hali mbaya na hivyo kuhatarisha maisha ya polisi wetu wanaohudumu katika maeno mbalimbali. Lakini kwa kushughulikia tatizo hilo serikali yangu ilinunua magari 30 yanayowakinga polisi ambazo zimeboresha uwezo wao na kuitikia dharura."

    Serikali imetumia shilingi bilioni 7.7 kukondisha magari haya zaidi ya mia tano.

    Mpango wa kukondisha magari ya polisi badala ya kununua ulianzishwa na serikali mwaka 2013 ikiwa ni hatua ya kupunguza gharama zautunzaji wa magari

    Chini ya mpango huo ambao sasa uko kwenye awamu ya 3 zaidi ya magari 2700 yamekondishwa kutoka kwa makampuni mbali mbali.

    Na hatua hii imezaa matunda kama anavyoeleza rais Uhuru Kenyatta.

    "Usalama umeimarika sana mjini Nairobi, matukio ya wizi yalipungua kutoka 436 zilizoripotiwa mwaka 2014 hadi 295 mwaka 2015. Wizi wa magari nao umepungua 340 hado 105. Aidha visa vidogo vidogo vya wizi vimeshuka kutoka 3, 360 mwaka 2014 hadi 900 mwaka 2016. Mafanikio hayo ya mjini Nairobi ni ishara wazi kwamba uwekezaji wa serikali yangu kwenye kamera za usalama na taa za barabarani unazaa matunda"

    Wakati akiwasilisha rasmi magari haya kwa polisi rais uhuru Kenyatta pia aliwataka wanasiasa kujiepusha na matamshi yanayoweza kusababisha chuki miongoni mwa araia wakati huu ikielekea uchaguzi mkuu mwezi Agosti baadaye mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako