• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China akutana na mwenyekiti wa Olimpiki ya kimataifa

    (GMT+08:00) 2017-01-18 20:15:45

    Rais Xi Jinping wa China leo amekutana na mwenyekiti wa Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa Thomas Bach kwenye Jumla la Makumbusho ya Olimpiki ya Kimataifa mjini Lausanne, nchini Uswisi.

    Kwenye mazungumzo yao, rais Xi ameshukuru kwa mchango mkubwa uliotolewa na Bw. Bach na mwenyekiti wa heshima Jacques Rogge kwa maendeleo ya michezo ya Olimpiki duniani na pia usaidizi wao kwa sekta ya michezo ya China. Amesema China inaunga mkono kithabiti michezo ya Olimpiki na kwamba Beijing itakuwa ni mji wa kwanza kuandaa michezo ya Olimpiki ya majira ya joto na pia utaandaa michezo hiyo ya majira ya baridi.

    Bw. Bach amesema Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa na jamii ya kimataifa zinatarajia michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi kufanyika mwaka 2022 mjini Beijing, na pia zina imani kuwa China itapata maendeleo makubwa zaidi kwenye sekta ya siasa, uchumi, utamaduni na michezo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako