• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Van Gaal asema hajastaafu kufunza soka

    (GMT+08:00) 2017-01-19 10:20:26

    Aliyekuwa meneja wa Manchester United Louis Van Gaal amesema hajastaafu na kwamba anachukua likizo ya mda. Van Gaal mwenye umri wa miaka 65 hajajiunga na timu nyengine tangu aondoke Old Trafford mnamo mwezi Mei.

    Siku ya Jumatatu, gazeti moja la Uholanzi De Telegraaf lilisema Van Gaal amemaliza muda wake wa ukufunzi na amestaafu kama mkufunzi, hatua iliyoshinikizwa na kifo cha mwanawe.

    Lakini alikiambia kituo kimoja cha redio nchini Uhispania Cadena Ser kwamba ijapokuwa kustaafu kunawezekana bado hajaamua. Raia huyo wa Uholanzi pia alibainisha kuwa amekataa kuifunza klabu ya Uhispania Valencia mwezi uliopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako