• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi akutana na mwenyekiti wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa na katibu mkuu wa Umoja huo

    (GMT+08:00) 2017-01-19 10:46:41

    Rais Xi Jinping wa China jana huko Geneva alikutana na mwenyekiti wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa Bw. Peter Thomson na katibu mkuu wa Umoja huo Bw. Antonio Guterres, na kusisitiza kuwa China inashikilia utaratibu wa kimataifa wenye ncha nyingi, kulinda katiba na kanuni za Umoja wa mataifa na kuuunga umoja huo utoe mchango mkubwa zaidi katika kulinda amani ya dunia na kuhimiza maendeleo ya pamoja.

    Bw. Thomson na Bw. Guterres wamesema China imefanya kazi muhimu ya uongozi kwenye kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, kupunguza umaskini, kuhimiza maendeleo endelevu na kulinda amani ya dunia. Wamesisitiza kuwa Umoja wa Mataifa unapenda kushirikiana na China katika kuhimiza amani na maendeleo ya dunia na kutimiza ndoto kubwa ya kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja.

    Siku hiyo, Rais Xi pia alitembelea makao makuu ya Shirika la afya duniani WHO na kukutana na katibu mkuu wa shirika hilo Bibi Margaret Chan, ambapo walishuhudia kwa pamoja kusainiwa kwa makubaliano ya ushirikiano wa afya kati ya serikali ya China na WHO katika mpango wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako