• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi za Afrika Mashariki zachukua tahadhari ya mafua ya ndege baada ya Uganda kukumbwa na ugonjwa huo

    (GMT+08:00) 2017-01-19 10:50:15

    Nchi za Afrika Mashariki zimeanza kuchukua tahadhari siku chache baada ya mlipuko wa homa ya mafua ya ndege kugunduliwa nchini Uganda.

    Serikali ya Tanzania inajiandaa kuunda timu ya wataalamu kutathmini hali ya ugonjwa huo katika Kanda ya Ziwa. Rwanda pia imetangaza hali ya tahadhari, na sasa wizara ya afya ya nchi hiyo inashirikiana na mashirika husika kuangalia kwa karibu hali ya ugonjwa huo na kuchukua hatua kuuzuia ugonjwa huo usiingie Rwanda.

    Kenya imetaka idara husika kufuatilia na kudhibiti homa hiyo, na kutoa mwito kwa wakenya kutangaza mapema iwezekanavyo kama wakigundua vifo visivyo vya kawaida vya ndege au kuku.

    Nchi tatu za Afrika mashariki Tanzania, Kenya na Rwanda zote zimetangaza marufuku ya kuagiza ndege kutoka Uganda na nchi nyingine za Ulaya zinazowezekana kukumbwa na ugonjwa huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako