• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Wanaonunua kutoka kwa wachuzi Rwanda kutozwa faini

    (GMT+08:00) 2017-01-19 19:00:01

    Mamlaka mjini Kigali nchini Rwanda imesema itawakama watu wanaonunua bidhaa kutoka kwa wachuuzi.

    Mamlaka wanasema sasa hawatawalenga wachuuzi wenyewe bali wateja kwenye hatua ya kuondoa desturi ya biashara haramu kwenye eneo la mji.

    Yeyote atayepatikana akinunua kutoka kwa wachuuzi atatozwa franc10,000 .

    Naibu meya Patricia Muhongerwa, ambaye pia anashughulikia maswala ya kijamii amesema wanawataka wachuuzi kujiunga kwa vikundi ili kufaidika na mipango inayotolewa na serikali badala ya kufanya biashara kwenye maeneo yaliokatazwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako